Dodoma FM

Manchali watakiwa kuwa walinzi wa vifaa vya ujenzi wa shule

18 September 2023, 11:03 am

Picha ni ujenzi wa Shule Mpya ya Kata ya Manchali,. Picha na Mariam Kasawa.

Huu ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi Mhe. Senyamule ambapo amekagua pia Ujenzi wa Mradi wa Shule Mpya ya kata ya Manchali, Mradi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Dodoma na Chuo cha Veta.

Na Mindi Joseph.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka mafundi wanaojenga Shule ya Sekondari Manchali ifikapo Oktoba 30 wawe wamekamilisha ujenzi huo katika ubora unaotakiwa.

Mh. Senyamule ametoa maagizo hayo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua Miradi mbalimbali ya Ujenzi wa chuo cha Veta na Shule za Sekondari.

Sauti ya Mh. Senyamule.
Wananchi wa Kijiji hicho wametakiwa kuwa na umoja ili kurahisisha ufanisi wa utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ya Kijiji hicho.Picha na Mariam Kasawa.

Katika hatua nyingine Senyemule amewataka wananchi wa Manchali kuwa walinzi wa mradi huo.

Sauti ya Mh. Senyamule.

Faraja Bwire ambae ni Fundi wa Ujenzi wa shule hiyo amesema haya.

Sauti ya Faraja Bwire.