Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuwajali yatima na wajane

18 September 2023, 4:52 pm

Sheikh Rajab ameikumbusha jamii kukemea Matendo maovu ikiwemo Vitendo vya Udhalilishaji. Picha na Seleman Kodima.

Katika tukio hilo Jumuiya ya wanawake wakiislamu Tanzania JUWAKITA wilaya ya Dodoma ililenga kuwa pamoja na Wajane 50 na Yatima 100 ikiwa ni muendelezo wa Kutenda Matendo Mema kwa Jamii .

Na Seleman Kodima.

Jamii imekumbushwa kuwajali,Kuwasaidia na kuwatazama zaidi yatima na wajane ikiwa ni njia mojawapo ya Agizo la Mwenyezi Mungu .

Wito Huo umetolewa na Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab Shaban wakati wa tukio la kuwa kirimu wajane na Yatima katika Mazazi ya Mtume Mohamed liliondaliwa na Jumuiya ya wanawake wakiislamu Tanzania JUWAKITA wilaya ya Dodoma.

Sauti ya Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab Shaban

Aidha Sheikh Rajab ameikumbusha jamii kukemea Matendo maovu ikiwemo Vitendo vya Udhalilishaji ,ukatili wa kijinsia,na mapenzi ya jinsia moja ambapo amesema sio mambo lenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.

Sauti ya Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab Shaban
Sheikh Rajab ameikumbusha jamii kukemea Matendo maovu. Picha na Seleman Kodima.

Kwa upande wao Viongozi wa JUWAKITA Dodoma akiongozwa na Fatuma Hussein na Zabibu Juma  ambapo wamesema wameamua kufanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kukumbuka matendo ambayo walimrishwa kufanya na Mtume Mohamed  ya kuwajali na Yatima na Wajane.

Sauti za viongozi wa JUWAKITA