Dodoma FM

Jamii yatakiwa kutambua umuhimu wa kupima afya

13 September 2023, 2:47 pm

Balisho Eliya mtaalamu wa Afya kutoka jijini Dodoma akiongea na Dodoma Tv.Picha na Richald Ezekiel.

Wataalamu wa Afya wanashauri jamii kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kubaini hali zao na namna ya kukabiliana na magonjwa yanayoweza kujitokeza kwa haraka zaidi .

Na Richald Ezekiel.

Jamii imetakiwa kutambua umuhimu wa kupima afya mara kwa mara ili kubaini magonjwa yanayoweza kujitokeza na namna ya kukabiliana nayo kabla hayajaleta madhara makubwa.

Akizungumza na Dodoma TV Balisho Eliya Balisho ambaye ni mtaalamu wa Afya kutoka jijini Dodoma, amesema kuwa upimaji huo wa afya humuwezesha mtu kuitambua hali ya afya yake na kupata kinga mapema kabla ya tiba.

Sauti ya Balisho Eliya.

Baadhi ya wanachi waliozungumza na kituo hiki juu ya upimaji wa afya zao wamekuwa na maoni tofauti kuhusu suala hilo.

Sauti ya za wananchi.