Dodoma FM

Vijana watakiwa kuacha tabia ya kutazama picha za utupu

12 September 2023, 3:02 pm

Picha ni mwanasaikolojia kutoka jijini Dodoma daktari Malaki Balage katika mahojiano maalum na Dodoma Tv.Picha na Thadei Tesha.

Kwa mujibu wa mwanasaikolojia huyo anasema kuwa zipo athari mbalimbali ambazo zinaweza kusababishwa na suala hilo ambapo wanashauri jamii hususani vijana kuachana na tabia hiyo.

Na Thadei Tesha.

Wito umetolewa kwa Wananchi hususani vijana kuepukana na tabia ya kuangalia picha za utupu mitandaoni kwani kwa kufanya hivyo zinaweza kusababisha athari za kisaikolojia.

Hayo yamesemwa na mwanasaikolojia kutoka jijini hapa daktari malaki Balage katika mahojiano maalum na dodoma tv

Amesema kuwa tabia ya baadhi ya vijana kutazama picha za utupu mitandaoni sio sahihi kwani zinaweza kuleta athari kisaikolojia na vitendo visivyo na maadili kwa jamii .

Sauti ya Dkt Malaki Balage.
Picha ni baadhi ya Vijana wakieleza hali inayopelekea wao kutazama picha za utupu. Picha na Thadei Tesha.

Aidha hapa anatumia fursa hii kutoa ushauri kwa vijana juuu ya namna wanaweza kuepukana na tabia hiyo.

Sauti ya Dkt Malaki Balage.

Dodoma Tv imefanya mahojiano na baadhi ya vijana wa mtaa wa mipango Jijini Dodoma ambapo hapa wanaeleza sababu inayopelekea vijana wengi kutazama picha za utupu mitandaoni.

Sauti za baadhi ya vijana.