Dodoma FM

Watumiaji wa vyombo vya usafiri walalamika kusimamishwa muda mrefu

6 September 2023, 12:52 pm

Picha ni baadhi ya madereva wa vyombo vya moto ikiwemo daladala na pikipiki wakilalamika kusimama muda mredu kusubiri misafara ya viongozi ipite. Picha na Khadija Ayoub.

Kwa mujibu wa wakazi wa Jiji la Dodoma wanasema kuwa mara nyingi changamoto ya foleni Jijini hapa husababashwa na misafara ya viongozi na kuchangia kukaa muda mrefu kandokando ya barabara wakingoja misafara kupita.

Na Khadija Ayoub.

Watumiaji wa vyombo vya usafiri Mkoani Dodoma wakiwemo madereva wamesema mwenendo wa kusimamishwa muda mrefu barabarani ili kupisha misafara ya viongozi inawaathiri katika shughuli zao za kila siku.

Dodoma TV imepita katika maeneo mbalimbali Jijini Dodoma na kuzungumza na baadhi ya Wananchi ambapo wanaeleza namna changamoto hiyo inavyowaathiri.

Sauti za wananchi.
Utaratibu wa kufunga barabara kwa muda mrefu ili kupisha misafara ya viongozi hatua ambayo kuchangia usumbufu kwa Wananchi. Picha na Khadija Ayoub.

Baadhi ya Madereva wa vyombo vya usafiri ikiwemo magari na pikipiki nao wamekuwa na haya ya kusema.

Sauti za baadhi ya madereva.

April 13 mwaka huu makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akizungumza na wakazi wa Kisesa Mkoani Mwanza alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi Nchini kuacha utaratibu wa kufunga barabara kwa muda mrefu ili kupisha misafara ya viongozi hatua ambayo kuchangia usumbufu kwa Wananchi.

Sauti ya Dkt. Philip Mpango