Dodoma FM

Watoto wasaidiwe kuvuka barabara ili kuepusha ajali

5 September 2023, 3:35 pm

Picha ikimuonesha mzazi akimsindikiza mtoto wakati wa kuvuka barabara kwenda shuleni. Picha na Thadei Tesha.

Kundi la watoto ni miongoni mwa makundi yanayohitaji misaada hususani pale wanapokuwa katika maeneo ya barabara ili kuepukana na ajali zinazoweza kutokea.

Na Thadei Tesha.

Jamii imetakiwa kushiriki katika suala la kuwasadia watoto pale wanapoelekea shuleni na maeneo mengine ya kijamii ili kuwaepusha na changamoto za barabarani ikiwemo ajali.

Dodoma tv imepita katika maeneo mbalimbali ingawa imeshuhudia uwepo wa watoto wakiwa na wazazi wao katika maeneo ya barabara lakini pia wapo baadhi ya watoto ambao wapo bila ya usimamizi wa wazazi.

Je wazazi wanashiriki vipi katika kuwaepusha watoto hawa dhidi ya ajali za barabarani?

Sauti za baadhi ya wazazi.
Picha ni baadhi ya wazazi wakiongea na Dodoma Tv . Picha na Thadei Tesha.

Aidha baadhi ya madereva wa vyombo vya usafiri ikiwemo magari na pikipiki nao hawapo nyuma katika kushiriki suala hili.

Sauti za baadhi ya Madereva.

Lakini sheria inasemaje kuhusu suala la kuwaangalia watoto pale wanapotumia barabara? Huyu hapa coplo Ester Makali mwalimu wa usalama barabarani anaeleza zaidi.

Sauti ya Koplo Ester Makali.