Dodoma FM

Jamii yatakiwa kufuata kanuni na taratibu ili kuepuka usugu wa dawa

5 September 2023, 3:10 pm

mfamasia kutoka jijini Dodoma bw. Pasko Kazana akieleza umuhimu wa kutumia dawa kwa usahihi.Picha na David Kavindi.

Matumizi holela ya dawa husababisha ugumu wa kutibu magojwa kutokana na mwili kuwa na usugu wa dawa.

Na David kavindi.

Jamii imeaswa kufuata kanuni na taaratibu za matumizi sahihi ya dawa ili kupeuka changamoto ya usugu wa dawa hizo mwilini. 

Dodoma Tv imefanya mahojiano na mfamasia kutoka jijini Dodoma bw. Pasko Kazana ambapo amesema ni muhimu kufuata taratibu kabla ya kutumia ya dawa kwa kuwaona wataalamu wa afya.

Sauti ya Pasko Kazana.
Picha ni aina mbalimbali za dawa katika duka la kuuzia dawa za binadamu jijini Dodoma.Picha na David Kavindi.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa matumizi holela ya dawa husababisha ugumu wa kutibu magojwa kutokana na mwili kuwa na usugu wa dawa.

Sauti ya Pasko Kazana.

Nao baadhi ya wakazi waishio jijini Dodoma wamezungumza na kituo hiki na kuzitaja sababu zinazo chochea baadhi yao kutumia dawa kiholela ikwemo ukosefu wa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa 

Sauti za baadhi ya wakazi.