Dodoma FM

DUWASA yaeleza mikakati yake ya kuboresha mfumo wa maji taka

30 August 2023, 5:25 pm

Wakazi Jijini Dodoma wameomba huduma hizo zikamilike kwa wakati kutokana na changamoto ya maji taka wanayoipataka katika makazi yao.Picha na Yussuph Hassan.

DUWASA inasema tayari bajeti imekwisha tengwa kwaajili ya kuanza ikaranbati huo.

Na Yussuph Hassan.

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma DUWASA, imeweka wazi mikakati yao katika kuhakikisha inaboresha mtandao wa maji taka ambapo tayari fedha imeshategwa kwa ajili ya maboresho hayo.

Edwin Muijage Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano DUWASA, amesema kuwa Serikali inaenda kuboresha huduma zilizopo Jiji la Dodoma na kuyafikia maeneo ambayo hakuna huduma hiyo.

Sauti ya Bw, Edwin Muijage.
Picha ni uzibuaji wa mitaro hiyo ya maji taka ukiwa unaendelea. Picha na Yussuph Hassan.

Aidha wanaendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mfumo wa maji taka.

Sauti ya Bw. Edwin Muijage.

Kwa upande wao Wakazi Jijini Dodoma wameomba huduma hizo zikamilike kwa wakati kutokana na changamoto ya maji taka wanayoipataka katika makazi yao.

Sauti ya wakazi wa jijini Dodoma.