Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuzingatia unywaji wa maji kwa kiwango kinachohitajika

29 August 2023, 5:11 pm

Ni muhimu kwa wanajamii kuzingatia unywaji wa maji kwa kiwango kinachohitajika ili kuepuka athari mbaya zinazowezakujitokeza kiafya. Picha na Google.

Hata hivyo, hii inaweza kutofautina kulingana na umri wako, jinsia na kiwango cha shughuli unayoifanya.

Na Abraham Mtagwa.

Imeelezwa kuwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hasa uwepo wa jua kali nyakati za mchana, ni muhimu kwa wanajamii kuzingatia unywaji wa maji kwa kiwango kinachohitajika ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kiafya.

Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wananchi Jijini Dodoma kufahamu juu ya utaratibu binafsi waliojiwekea juu ya unywaji wa Maji kama moja ya kitu muhimu sana katika mwili wa mwanadamu huku wakieleza baadhi ya faida za kunywa maji ya kutosha.

Sauti za baadhi ya wananchi.

Aidha, kituo hiki kimezungumza na  Bw. Juma Ali ambaye ni mfanyabiashara wa maji ya kunywa kutoka soko la Machinga Complex Jijini Dodoma ili kufahamu hali ilivyo juu ya ununuaji wa maji hasa katika eneo hilo la soko ambalo lina mwingiliano mkubwa wa watu.

Sauti ya Bw. Juma Ali.

Kwa upande wake Bw. Stephano Daburu ambaye ni Mteknolojia na Mtaalamu wa Afya kutoka Jijini Dodoma, ameikumbusha Jamii juu ya unywaji wa Maji kwa Kiwango kinacho hitajika ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ukosefu wa Maji ya kutosha Mwilini.

Sauti ya Bw. Stephano Daburu

Vilevile Bw. Daburu ametoa ushauri kwa watu wenye utaratibu wa kutumia maji wakati wa kula chakula kuacha utaratibu huo kwani sio mzuri sana kiafya.

Ikumbukwe, maji safi na usafi wa mazingira ni moja ya malengo endelevu ya maendeleo duniani,  Shirika la Huduma ya Afya ya Umma ya Uingereza (NHS),  linapendekeza mtu mzima kunywa wastani wa glasi 6-8 za maji kila siku.