Dodoma FM

Serikali yakamilisha ujenzi wa minara 304 ndani ya Mwaka mmoja.

28 August 2023, 5:45 pm

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeendelea kutekeleza miradi ya mawasiliano ambapo imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 205.9 ikiwa ni mchango wa Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya huduma za mawasiliano vijijini. Picha na UCSAF

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF)  unaendelea na ukaguzi wa minara yote iliyowashwa ili kuona utendaji kazi wake unakidhai vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Mikataba

Na Selemani Kodima

Katika kuendelea kutatua changamoto za mawasiliano nchini  ,Serikali  imefanikiwa kukamilisha  miradi ya mawasiliano  vijijini  kwa mwaka wa mmoja wa fedha Julai  2022 hadi Juni 2023 kwa kujenga minara 304.

Minara hiyo imejengwa katika kata 291 ndani ya vijiji 580 ambapo jumla ya wananchi 3,343,565 wamenufaika na miradi hiyo.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(yuuksaf SAF) imeeleza kuwa  kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai 2022-juni 2023 jumla ya minara 304 imejengwa.

Ili kuongeza matumizi ya intaneti nchini kama ilivyoainishwa katika  Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, UCSAF imeendelea kutekeleza mradi  ujenzi wa Minara .Picha na UCSAF

Aidha UCSAF imeeleza kuwa miradi iliyokamilika katika kipindi hicho ni pamoj na TTCL imefanikiwa kuwasha minara 72,VODACOM minara 17,AIREL minara  33 ,HALOTEL minara 123 na MIC minara 59.