Dodoma FM

Mapato ya ndani kukamilisha kituo cha afya Nagulo Bahi

21 August 2023, 5:58 pm

Picha ni majengo ya Zahanati ya Nagulo akiwa katika hatua mwisho ya ukamilishaji.Picha na Mindi Joseph.

Kituo hicho cha afya kimetumia mapato ya ndani katika ujenzi wake huku wananchi wakichangia milion 6 na Mbunge wa jimbo hilo akichangia milion 6.

Na Mindi Joseph.

Jumla ya shilingi milion 62 zimetumika katika ujenzi wa kituo cha afya wilayani Bahi huku shilingi milioni 50 za mapato  ya ndani ya halmashauri zikitarajiwa kutumika kukamilisha ujenzi huo.

Ujenzi wa kituo hicho umekamilishwa na wananchi baada ya kushiriki kutoa nguvu zao na michango

Diwani wa kata ya Bahi Augustino Ndonu amesema wananchi walichangia milioni 6 kama anavyozungumza.

Sauti ya Augustino Ndonu.
Ujenzi wa kituo hicho upo hatua za mwisho kuweza kukamilika na kurahisisha huduma za Afya kwa wananchi. Picha na Mindi Joseph.

Dkt. Izack Adina Mratibu wa Mfuko wa Jamii CHF wilaya ya Bahi anasema ni wakati wa wananchi kujiunga kwenye mfuko wa afya ya Jamii ili wapate huduma kwa urahisi pindi kituo hicho kitakapoanza kutumika.

Sauti ya Dkt Izack Adina.