Dodoma FM

Viongozi wa dini watakiwa kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali

15 August 2023, 1:18 pm

Mchungaji kiongozi wa Kanisa  Sinai EAGT Meshack Mwakyoma akizungumza katika semina hiyo.Picha na Seleman Kodima.

Viongozi pia wamekumbushwa kuendelea kuliombea Taifa.

Na Seleman Kodima.

Wito umetolewa kwa watumishi na Viongozi wa Dini kuwa na Moyo wa kusaidiana watu wenye mahitaji mbalimbali pindi wanapokuwa kwenye majukumu ya  utumishi.

Wito huo umetolewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Sinai EAGT  Njedengwa  Filbert Edward  wakati akifunguwa Semina ya Siku Saba iliyofanyika kanisani hapo .

Sauti Mchungaji Filbert Edward.
Kutoa misaada kwa watu mbalimbali ni kueneza injili kwa upendo.Picha na Seleman Kodima.

Pia amewakumbusha Viongozi wa Dini  wanapofanya Mikutano mbalimbali kuhakikisha wanaendelea kuliombea taifa kutokana Mwenendo wa Matukio yanayojiri Duniani ikiwemo Vitendo vya Mapenzi ya Jinsia moja.

Sauti ya Mchungaji Filbert Edward.

Kwa upande mwingine ,Mchungaji kiongozi wa Kanisa  Sinai EAGT Meshack Mwakyoma amesema lengo la kutoa msaada vitu mbalimbali kwa watu wenye mahitaji ni kuendelea kueneza injili kwa njia ya Upendo na kuwajali wengine.

Sauti ya mchungaji Meshack Mwakyoma.