Dodoma FM

Rushwa ya ngono inavyowaathiri vijana katika utafutaji

14 August 2023, 12:41 pm

Baadhi ya vijana wanasema wamekuwa wakikumbwa na changamoto hii ya kuombwa rushwa ya ngono pale wanapokuwa wanahitaji kufanikiwa kimaisha. Picha na Habari leo.

Nini kifanyike ili kuwanusuru vijana pindi wanapokutana na changamoto ya kuombwa rushwa ya ngono.

Na Leonard Mwacha.

Vijana wamekuwa wakipitia changamoto nyingi pindi wanapotafuta maisha ikiwemo kuombwa rushwa ya ngono ili waweze kufanikiwa kimaisha.

Hali hii imekuwa ikiwakatisha tamaa vijana wengi na kufanya kushindwa kuendelea katika utafutaji hasa wanapokutana na changamoto hii ambayo mara nyingi huishia kuwaumiza wasiokubaliana nayo.