Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuwapatia haki ya elimu watoto wenye ulemavu

10 August 2023, 1:20 pm

Ufuatiliaji wa watoto wenye ulemavu umeendelea wilayani Bahi kwani watoto zaidi ya 30 wenye ulemavu wameibuliwa baada ya  kufungiwa ndani. Picha na Mariam Kasawa.

Ingawa malengo ya maendeleo endelevu yanahimiza kuwa hakuna mtoto anayepaswa kuachwa nyuma lakini utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumiwa Watoto UNICEF 2022 unaonesha kuwa kati ya watoto milioni 240 wenye ulemavu duniani nusu hawajawahi kuhudhuria shuleni.

Na Mindi Joseph.

Wanafunzi wilayani Bahi wamepaza sauti zao kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu kuwapa haki ya elimu watoto hao na kuacha kuwafungia  ndani.

Desturi ya kuwaficha watoto wenye ulemavu imeendelea kuonekana katika jamii  na kupelekea watoto hawa kukosa elimu.

Elimu ni ufunguo wa maisha na kila mtoto ana haki ya kupata elimu kama wanavyosema wanafunzi wa shule ya msingi Bahi.

Sauti za wanafunzi.
Picha ni mwanafunzi wa shule ya msingi akieleza kuhusu haki za watoto. Picha na Mariam Kasawa.

Ufuatiliaji wa watoto wenye ulemavu umeendelea wilayani Bahi kwani watoto zaidi ya 30 wameibuliwa baada ya  kufungiwa ndani kama anavyosema Diwani Kata ya Bahi Mkoani Dodoma Mhe.Augustino Ndonu.

Sauti ya Diwani wa kata ya Bahi.