Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuondokana na matumizi holela ya dawa

10 August 2023, 12:45 pm

Matumizi holela ya dawa husababisha madhara katika mwili wa binadamu.Picha na Thadei Tesha.

Kwa Mujibu wa Mtaalamu Teobad Abdon ameeleza kuwa matumizi holela ya dawa husababisha madhara katika mwili wa binadamu ikiwemo matumizi ya dawa ambazo sio za ugonjwa husika.

Na Diana Massae.                                                                                      

Jamii imetakiwa kuondokana na matumizi holela ya dawa bila kuzingatia vipimo sahihi kutoka kwa daktari.

Kauli hiyo imetolewa na Tabibu Teobadi Abdon kutoka Cohaso jijini Dodoma wakati akizungumza na Dodoma Tv huku akisisitiza kuwa Ni vyema jamii ikazingatia matumizi sahihi ya dawa ili kuepukana na madhara mbalimbali ya kiafya.

Sauti ya Tabibu Teobadi .
Tabibu Teobadi Abdon kutoka Cohaso jijini Dodoma akiongea na Dodoma Tv. Picha na Thadei Tesha.

Baadhi ya wakazi wa Jijini Dodoma wakizungumza na kituo hiki meeleza sababu kuu inayosababisha matumizi ya dawa pasipo kuchukua vipimo ni kutokana na ucheleweshwaji wa huduma katika vituo vyakutolea huduma za afya pamoja na kutokukidhi gharama za matibabu.

Sauti za wananchi.