Dodoma FM

Wananchi waelimishwa utunzaji wa vyanzo vyanzo vya maji

8 August 2023, 3:22 pm

Wananchi wameendelea kupewa elimu ya kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji ili kunusuru vyanzo hivyo. Picha na Mindi Joseph.

Licha ya kuwepo kwa Sheria za Usimamizi wa vyanzo vya maji bado umekuwepo uharibifu wa vyanzo vya maji kutokana na kuwepo kwa shughuli za kibinadamu zinazofanyika pasipo kuzingatia Sheria zinazosimamia mazingira na rasilimali maji.

Na Mindi Joseph.

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuacha kuvamia na kuharibu vyanzo vya maji.

Mhandisi Mazingira Ruwasa Ofisi ya Meneja Mkoa wa Dodoma  Neema Massawe amesema wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kuzingatia kutokufanya Shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.

Ameongeza kuwa uharibifu wa mazingira husababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji na kupoteza muonekano na matumizi ya awali.

Sauti ya Mhandisi Mazingira Ruwasa Ofisi ya Meneja Mkoa wa Dodoma
Uchafuzi wa vyanzo vya maji unachangiwa na uharibifu wa mazingira. Picha na Mindi Joseph.

Wenyeviti wa serikali za mitaa wanafanya jitihada gani katika kuhimiza wananchi kulinda vyanzo ya maji huyu ni Mwenyekiti wa mtaa wa Mtumbe Dodoma John Masaka anaeleza.

Sauti ya mwenyekiti