Dodoma FM

Utandawazi, mitindo ya maisha vyatajwa kuathiri unyonyeshaji

7 August 2023, 1:28 pm

Utandawazi na mitindo ya maisha vyatajwa kuathiri unyonyeshaji. Picha na Mariam Msagati.

Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yamezinduliwa Agosti Mosi mwaka huu na kilele chake ni Agosti 08.

Na Mariam Msagati.

Baadhi ya wananchi jijini Dodoma wameelezea kuwepo kwa sababu mbalimbali zinazochangia baadhi yao kushindwa kunyonyesha watoto ipasavyo.

Wakizungumza na Dodoma TV wananchi hao wamesema kutokana na kushamiri kwa utandawazi na mitindo mbalimbali ya maisha imesababisha baadhi ya akina mama kushindwa kunyonyesha watoto wao ipasavyo.

Sauti za baadhi ya wananchi.
“Mabinti wa Sasa hawana elimu ya unyonyeshaji hawafahamu hata jinsi ya kumuweka mtoto vizuri wakati wa kumnyonyesha” anasema Bi Latifa Abdala makazi wa jijini hapa. Picha na Mariam Msagati.

Bi Clara Njenjema pamoja na Bi Asha Shabani ni miongoni mwa akina mama ambao wameeleza tofauti ya maisha ya sasa na ya miaka ya nyuma katika utekelezaji wa zoezi la unyonyeshaji wa watoto.

Sauti za wananchi.

Miongoni mwa wananchi waliozungumza na kituo hiki wamesisitiza umuhimu wa elimu kutolewa mara kwa mara kwa jamii ili kuhakikisha watoto wananyonyeshwa ipasavyo.