Dodoma FM

Ujenzi bweni la wasichana Mpendo wafikia hatua za mwisho

2 August 2023, 1:57 pm

Picha ni Bweni hilo la wasichana katika shule ya sekondari Mpendo.Picha na Mindi Joseph.

Ujenzi huo upo hatua za mwisho na mwezi huu wa nane wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne wataanza kulitumia.

Na Mindi Joseph.

Ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Mpendo kata ya Mpendo wilayani Chemba umetajwa kutatua changamoto ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wa kike.

Mkuu wa shule ya sekondari Mpendo Ginelu Gisilu anasema kabla ya ujenzi huu kufanyika wanafunzi wa kike walikuwa wanapata changamoto kubwa .

Sauti ya Mkuu wa shule.
Ujenzi wa bweni hilo unatajwa utapunguza tatizo la mimba kwa wanafunzi .Picha na Mindi Joseph.

Kwa upande wa diwani wa kata ya Mpendo Bernad Kapaya anasema ujenzi wa bweni ulianza mwaka 2020.

Sauti ya Diwani wa Mpendoo.

Milioni zaidi ya 110 zimetumika katika ujenzi wa bweni hadi kukamilika kwake.