Dodoma FM

Uwekezaji wa bandari ni chanzo cha mapato ya nchi

1 August 2023, 3:29 pm

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dodoma Pili Mbaga wakati akihutubia katika ibada ya kuwasimika kazini maaskofu wateule wa kanisa la kiinjili la utatu mtakatifu. Picha na Pius Jayunga.

Maaskofu walioapishwa ni pamoja na Askofu Simon Maloda wa Dayosisi ya Dodoma, Askofu Leoanard Matia Mbole wa Dayosisi Bahi.

Na Pius Jayunga.

Uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam umetajwa kuwa chanzo mojawapo cha ukusanyaji wa mapato ya nchi ili kuiwezesha serikali kufanikisha azma ya kuwahudumia wananchi.

Hayo yamesemwa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dodoma Pili Mbaga wakati akihutubia katika ibada ya kuwasimika kazini maaskofu wateule wa Kanisa la Kiinjili la Utatu Mtakatifu lililopo kata ihumwa jijini Dodoma.

Amesema iwapo mkataba huo utapitishwa utasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka trilioni 7 hadi trilioni 27 kwa mwaka.

Sauti ya katibu wa CCM mkoa wa Dodoma.

Askofu David Matonya wa kanisa la Free Anglikana kutoka Singida amewataka viongozi wa dini kuwa chanzo cha amani ndani na nje ya kanisa.

Sauti ya Askofu David Matonya wa kanisa la Free Anglikana kutoka Singida
Picha ni waumini wa kanisa hilo la utatu mtakatifu wakifatilia zoezi hilo. Picha na Pius jayunga

Maaskofu walioapishwa katika ibada hiyo wameahidi kutoa kushirikiano kwa viongozi wa serikali pamoaj na kanisa katika kuhudumia jamii inayowazunguka.

Sauti za maaskofu walio apishwa

Ifahamike kuwa kanisa la kiinjili la utatu mtakatifu lilianzishwa 2007 na muasisi wake askofu kuwayawaya steven kuwayawaya na hadi sasa kanisa hilo lina jumla ya maaskofu watatu.