Dodoma FM

NIRC kujenga mabwawa 100 nchi nzima

31 July 2023, 5:34 pm

Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Bw.Raymond Mndolwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wake Kwa Mwaka huu wa fedha.Picha na Seleman Kodima.

Hatua hiyo itafanya kuwa na  mabwawa 114 ambayo yatawasaidia wakulima kuwa na Kilimo Cha uhakika.

Na Seleman Kodima.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC imewahakikishia wananchi kuwa hakuna mradi wowote umesimama kwa sababu ya fedha bali zipo hatua ambazo lazima zifuatwe.

Pia tume hiyo imesema kuwa inatarajiwa  kujenga mabwawa 100 nchi nzima katika mwaka wa fedha 2023/24  ili kusaidia wakulima kuweza kulima zaidi ya vipindi viwili.

Hatua hiyo itafanya kuwa na  mabwawa 114 ambayo yatawasaidia wakulima kuwa na kilimo cha uhakika.

Hayo yamesemwa kwa mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Bw. Raymond Mndolwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wake kwa mwaka huu wa fedha.

Sauti ya Mkurugenzi.
Picha ni ujenzi wa bwawa la Membe linalojengwa Wilayani Chamwino jijini Dodoma.Picha na Msumba News.