Dodoma FM

Wadau wa mazingira watakiwa kuanza kuandaa vitalu vya miti

28 July 2023, 1:11 pm

Zoezi la upandaji miti katika shule ya sekondari Lukundo jijini Dodoma lililofanyika hapo jana likiongozwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma. Picha na Seleman Kodima.

Ama kweli penye nia pana njia haijalishi ni kianganzi ama masika lakini zoezi la upandaji miti limeendelea kufanyika.

Na Mindi Joseph.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amewaomba wadau wa mazingira kuanza kuandaa vitalu vya upandaji miti kwa msimu wa mvua unaokuja.

Shekimweri amewaongoza wadau wa mazingira kupanda miti 200 katika shule ya sekondari Lukundo ambapo zoezi hilo limeratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Green Home.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri akizungumza na wadau wa mazingira, walimu na wanafunzi wa Lukondo sekondari baada ya zoezi la upandaji miti shuleni hapo. Picha na Seleman kodima.

Mkuu wa shule ya sekondari Lukundo ameomba kujengewa uzio ili kulinda miti iliyopandwa na kwa usalama wa wananfunzi huku mkurugenzi wa shirika la Green Home akibainisha lengo la shirika hilo kupanda miti ndani ya shule hiyo ya sekondari.

Sauti za Mkuu wa shule na Mkurugenzi wa shirika la Green home.

Wanafunzi wanasema ni faraja kwao kuona miti inapandwa katika shule yao.

Sauti za wanafunzi wa Lukundo Sekondari.

Shule ya Sekondari Lukundo ina jumla ya wanafunzi 1365.