Dodoma FM

Fahamu shughuli zinazofanyika bwawa la Hombolo

28 July 2023, 5:07 pm

Picha ni wavuvi wakivuta nyavu zao za kuvulia samaki kutoka katika bwawa hilo. Picha na Fahari ya Dodoma.

Je bwawa hili linawanufaisha vipi wakazi wa Hombolo hususani katika shughuli mbalimbali kama kilimo na uvuvi?

Na Yussuph Hassan.

Bwawa la Hombolo limekuwa likitumika na wakazi wa eneo hilo kwa ajili ya uvuvi wa samaki aina ya perege na wengine wanaopatikana katika bwawa hilo kama vile kambale na uduvi . Baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wanatumia maji ya bwawa hilo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Picha ni muonekano wa bwawa hilo la Hombolo. Picha na Fahari ya Dodoma.