Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuunga mkono juhudi za kupinga vitendo visivyo na maadili

25 July 2023, 3:46 pm

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Fatina Majengo Bi Maua Mbaruku akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Aisha Shaban.

Mara kadhaa jamii imeendelea kuhamasishwa na serikali pamoja na taasisi mbalimbali juu ya umuhimu wa kufundisha maadili mema ndani ya jamii ili kujenga kizazi chenye misingi bora ya malezi.

Na Aisha Shaban.

Wananchi jijini Dodoma wametakiwa kuunga mkono juhudi za kupinga vitendo visisvyo na maadili kwa watoto ili kukuza malezi bora.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Fatina Majengo bi Maua Mbaruku ambapo amesema ni vyema wazazi kuendelea kukaa karibu na watoto wao na kuwapa elimu juu ya masuala mbalimbali kwa lengo la kutokomeza vitendo hivyo.

Sauti ya mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Fatina.
Mkazi wa Dodoma akizungumza na Dodoma Tv kuhusu kuunga mkono juhudi za kupinga maadili yasiyo faa. Picha na Aisha Shaban.

Aidha ameongeza kuwa ni vyema serikali ikashirikiana na wananchi katika utoaji wa elimu juu ya misingi ya maadili mema.

Sauti ya mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Fatina.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wamezungumza na kituo hiki na kushauri mbinu mbalimbali za kufanya ili kutokomeza vitendo viovu ndani ya jamii.

Sauti za wananchi.