Dodoma FM

Mikoa yote nchini yaagizwa kuadhimisha siku ya mashujaa

24 July 2023, 6:37 pm

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenister Mhagama pamoja na Waziri wa Ulinzi Innocent Bashungwa wakizungumza jambo katika uwanja huo. Picha na Mindi Joseph.

Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yamekamilika katika eneo la Mtumba jijini Dodoma huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kesho kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa eneo hilo.

Na Mindi Joseph.

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kesho Julai 25, mikoa yote nchini imeagizwa kufanya maadhimisho hayo ili kuendelea kutunza historia, kukuza na kuendeleza amani na mshikamano wa kitaifa.

Hatua hiyo ni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza kujengwa eneo la kumbukumbu lenye hadhi ya Makao Makuu kutokana na umuhimu wa siku hiyo badala ya kuendelea kulitumia eneo la mashujaa Jamatini jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenister Mhagama amesema siku hiyo ni muhimu kwa sababu inawakumbusha watanzania kwa ujumla kuhusu wajibu wao wa kutunza historia ya mashujaa waliopigania, kutetea na kulinda uhuru wa nchi.

Sauti ya Mh.Jenister Mhagama,
Picha ni Mnara wa Mashujaa ambao upo katika uwanja huo wa mashujaa.Picha na Mindi Joseph.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Innocent Bashungwa amewahimiza Wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Maadhimisho hayo.

Sauti ya waziri wa ulinzi.