Dodoma FM

Serikali yaendelea kuboresha miundombinu ya elimu nchini

21 July 2023, 3:10 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo shule ya sekondari Chilonwa. Picha na Mariam Kasawa.

Ziara hiyo ambayo ilianzia shule ya sekondari Chilonwa kwaajili ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na Mabweni ilihitimishwa shule ya Msingi mizengo pinda ambapo benki ya NMB ilikuwa ikikabidhi vifaa mbalibali vya ujifunzaji shuleni hapo iliwemo viti na vifaaa vingine.

Na Mindi Joseph.

Imeelezwa kuwa lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suuhu Hassani ni kuboresha miundombinu ya elimu Nchini na kuwezesha wanafunzi kupata elimu katika maeneo yao.

Ni katika ziara ambayo imefanyika katika wilaya ya Chameino kukagua ujenzi wa Vyumba vya madarasa, mabweni , matundu ya vyoo pamoja na utengenezaji wa viti na vifaa vitakavyo tumiwa na wanafunzi hao kama vile viti pamoja na vitanda .

ziara hiyo ambayo ilifika katika shule ya Msingi Mizengo Pinda iliyopo Chinangali two wilaya ya Chamwino na mkuu wa wilaya ya Chamwino  Gift Msuya amesema haya.

Sauti ya Mkuu wa wialaya ya Chamwino.
Baadhi ya vifaa vya shule ikiwemo viti na meza vilivyo kabidhiwa na NMB kwa shule ya msingi Mizengo Pinda. Picha na Mariam kasawa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule ambaye alikuwa mgeni rasmi kati ziara na hafla hiyo ya kupokea vifaa katika shule ya Msingi Mizengo Pinda amesema nia ya serikali ni kuboresha elimu nchini huku akiipongeza  benki ya NMB kwa kutoa msaada katika shule hiyo ya msingi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.