Dodoma FM

Jamii yatakiwa kushirikiana na wadau kuibua changamoto zilizopo katika shule

19 July 2023, 7:42 pm

AFNET limendelea kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za shule Mkoani Dodoma kuhusu uendeshaji na usimamizi wa shule.Picha na George John.

Shirika lisilo la kiserikali linalopinga ukatili wa kijinsia na watoto AFNET limendelea kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za shule mkoani Dodoma kuhusu uendeshaji na usimamizi wa shule ili kuleta maendeleo na kuboresha kiwango cha elimu.

Na Mindi Joseph.

Jamii imetakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu kuibua changamoto zilizopo katika shule ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

Thobias Mtui ni mratibu wa mradi  kutoka shirika la AFNET amesema bado kuna changamoto katika shule mbalimbali hivyo ni wakati wa kamati ya uwajibikaji jamii na jamii kushirikiana kuziibua.

Sauti ya mratibu wa mradi  kutoka shirika la AFNET.
Mwananchi akizungumza na Dodoma Tv kuhusu mkakati huo. Picha na George John.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka Maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma wamebainisha haya.

Sauti za baadhi ya wananchi.