Dodoma FM

Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wakandarasi wazawa

14 July 2023, 5:32 pm

Picha ni baadhi ya Wakandarasi na Wafanyabiashara walio hudhuria katika semina ya wakandarasi na wafanyabiashara iliyoandaliwa na moja ya benki nchini kwa lengo la kujadili namna ya kukuza uchumi kupitia miradi ya ujenzi. Picha na Ofisi ya mkuu wa Mkoa.

Wakandarasi wazalendo nchini wameiomba serikali kuwapatia miradi mikubwa ili kutoa ajira kwa watanzania wengi.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa  wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa serikali hasa ya Mkoa wa Dodoma itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wakandarasi wazawa huku akiwataka wakandarasi hao  kumaliza miradi wanayopewa kwa wakati

Mhe. Senyamule ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya wakandarasi katika semina ya wakandarasi na wafanyabiashara iliyoandaliwa na moja ya benki nchini kwa lengo la kujadili namna ya kukuza uchumi kupitia miradi ya ujenzi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule akizungumza na baadhi ya wakandarasi katika semina ya wakandarasi na wafanyabiashara.Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wakandarasi wazalendo nchini Bwana Thobias Kyando ameiomba serikali kuwapatia miradi mikubwa ili kutoa ajira kwa watanzania wengi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha wakandarasi wazalendo nchini.