Dodoma FM

Uchaguzi mdogo wa madiwani Tanzania bara kufanyika leo

13 July 2023, 12:00 pm

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akisoma risala ya uchaguzi hapo jana Jijini Dodoma. Picha na Mindi Joseph.

Upigaji kura unafanyika katika vituo vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 na mpiga kura aliyepoteza kadi au kadi yake kuharibika ataruhusiwa kutumia kitambulisho mbadala iwapo tu atakuwa ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura .

Na Mindi Joseph.

Wapiga Kura 74,642 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanashiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 13 za Tanzania Bara leo Julai 13,2023.

Jumla ya vyama vya siasa 17 vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo mdogo na wapiga Kura 74,642 wanashiriki katika uchaguzi huu mdogo huku vituo 205 vya kupigia kura vikitumika.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele ameyasema hayo jijini Dodoma katika Risala ya Uchaguzi huo mdogo unaofanyika kujaza nafasi wazi za udiwani.

Sauti ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Wasimamizi wa uchaguzi, vyama vya siasa na wagombea wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi wakati wa Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika Kata 13 za Tanzania Bara.

Sauti ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.