Dodoma FM

Wilaya ya Kondoa yaagizwa kulipa madeni ya watumishi umma

12 July 2023, 3:05 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule akizungumza katika baraza la Madiwani Kondoa. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Halmashauri hiyo imetakiwa kuhakikisha inalipa madeni yote ya watumishi wa umma kabla ya kupokea bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/24.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule ameiagiza halmashauri ya Kondoa kuhakikisha inalipa Madeni yote wanayodaiwa  na watumishi wa Umma katika halmashauri hiyo kabla ya kupokea fedha za bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/24

Mhe.Rosemary Senyamule  amaeyasema hayo wakati akisiriki katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini   kwa lengo la kujadili  taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa serikali katika halmashauri hiyo

Sauti ya Mkuu wa Mkoa.
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika baraza hilo la Madiwani. Picha na ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Aidha katika hatua nyingine Mh Rosemary ameipongeza halmashauri ya wilaya hiyo ya Kondoa vijijini kwa kupata hati safi Kwa ukaguzi wa  hesabu za serikali zinazoishia Juni 30 mwaka 2022.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa.