Dodoma FM

Wakazi wa Chang’ombe Kongwa waiomba serikali iwatatulie adha ya maji

11 July 2023, 1:10 pm

Kitongoji cha Chang’ombe kinachopatikana kata ya Laikala wilayani Kongwa. Picha na Mindi Joseph.

Changamoto ya maji imesalia kuwa kilio kwa wananchi pamoja na serikali kuendelea kufanya jitihada mbalimbali.

Na Mindi Joseph.

Wananchi wa kitongoji cha chang’ombe Kata ya Laikala Wilyani Kongwa wameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya maji inayowakabili.

Visima vilivyopo ni viwili huku kimoja kinatumika katika shughuli za kilimo.

Dodoma Tv imezungumza na Festo Elias mwenyekiti wa kitongoji cha chang’ombe kata ya Laikala ambapo amebainisha yafuatayo.

Sauti ya mwenyekiti wa kitongoji cha chang’ombe .
Festo Elias Mwenyekiti wa kitongoji cha chang’ombe kata ya Laikala akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Mindi Joseph.

Halima Sangula ni mkazi wa kitongoji hicho anasema msongamano wa wananwake katika kuchoa maji ni mkubwa.

Sauti ya Halima Sangula.