Dodoma FM

Wahudumu wa Afya nchini watakiwa kupunguza semina

11 July 2023, 4:45 pm

Waziri wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu akizungumza na wataallamu wa afya katika ziara yake Mkoani Simiyu. Picha na Wizara ya Afya.

Aidha Waziri Ummy amewataka wataalamu hao wa afya kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia kazi zao za tiba.

Na Fred Cheti.

Waziri wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu amewataka wataalamu wa afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo wakati akizungumza na wataallamu wa afya katika ziara yake Mkoani Simiyu ambapo amesema semina nyingi kwa wataalamu wa afya zimekuwa zikizorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Sauti ya Waziri wa Afya.

Aidha Waziri Ummy amewataka wataalamu hao wa afya kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia kazi zao za tiba.

Sauti ya Waziri wa Afya.