Dodoma FM

Biashara ya tangawizi, vitunguu swaumu yadoda Dodoma

10 July 2023, 4:49 pm

Viungo aina ya tangawizi na vitunguu saumu vimekuwa vikinunuliwa kwa wingi zaidi msimu wa sikukuu tofauti na siku za kawaida. Picha na Thadei Tesha.

Kwa sasa miongoni mwa viungo vinavyoonekena kushamiri katika masoko mbalimbali jijini Dodoma ni pamoja na vitunguu swaumu na tangawizi ambapo wengi wa wafanyabiashara hao wanasema kuwa msimu wa bidhaa hizo ni sasa kutoka mashambani.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wanaojishughulisha na kuuza viungo vya chai na chakula ikiwemo tangawizi pamoja na kitunguu saumu wamesema kuwa pamoja na uwepo wa bidhaa hizo kwa wingi sokoni lakini mwitikio wa wateja si wakuridhisha.

Dodoma tv imewatembelea baadhi ya wafanyabiashara hao ambapo wanasema kuwa ingawa kwa sasa ni upatikanaji wa bidhaa hiyo mashambani umeanza kuwa kwa kiasi kikubwa lakini kumekuwa na mwitikio mdogo wa wateja kuja kununua bidhaa hizo.

Sauti za wafanyabiashara.
Mfanyabiashara wa viungo kutoka soko kuu Majengo Jijini Dodoma akiongea na Dodoma Tv. Picha na Thadei Tesha.

Aidha wameongeza kuwa wateja wengi wa bidhaa hizo hujitokeza kununua kwa wingi bidhaa hizo hasa msimu wa sikukuu hapa Dodoma tv imewauliza baadhi ya wateja juu ya kwa nini mwitikio wa kununua bidhaa hizo sokoni si wa kuridhisha?

Sauti za wafanyabiashara.