Dodoma FM

Msimu wa mavuno, bei ya mchele yashuka sokoni

7 July 2023, 6:12 pm

Mfanyabiashara wa mchele kutoka soko kuu Majengo jijini Dodoma akizungumza na Dodoma Tv . Picha na Thadei Tesha.

Kwa sasa wastani wa bei ya mchele sokoni ni kati ya shilingi 2,300, 2,500 na kuendelea ambapo hapo awali ilikuwa kati ya shilingi 3,000, 3,500 na kuendelea na kwa mujibu wa wafanyabiashara wanasema kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kumetokana na msimu wa mavuno.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mchele jijini Dodoma wamesema kwa sasa bei ya mchele imeendelea kushuka ukilinganisha na kipindi cha nyuma kabla ya msimu wa mavuno.

Dodoma tv imewatembelea baadhi ya wafanyabiashara wa mchele jijini Dodoma ambapo kwanza nilianza kwa kuwauliza hali ya bei ya bidhaa hiyo kwa sasa ipoje na hapa wanaeleza.

Sauti za wafanyabiashara wa mchele.
Picha ni bei mbalimbali za Mchele sokoni Majengo. Picha na Thadei Tesha.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wanasema kuwa kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kumerahisisha na kupunguza changamoto iliyokuwa ikIwakumba ya kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo ambapo awali ilikuwa ikiuzwa kati ya shilingi 3000 na kuendelea.

Sauti za Wanunuzi.