Dodoma FM

Halmashauri yaeleza mikakati yake ya kutatua migogoro ya ardhi

7 July 2023, 1:03 pm

Kaimu Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Godwin Gondwe wakati akitoa tamko la jiji kwa waandishi wa habari.Picha na Fred cheti.

Itaundwa timu ya wataalam wa ardhi wa jiji la Dodoma kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi hao ambayo itakaa ndani ya siku 7 na kupitia maeneo mbalimbali ya mgogoro.

Na Fred Cheti.

Halmashauri ya jiji la Dodoma imesema moja ya mikakati yake ni kutatatua migogoro yote ya masuala ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya jiji hili ili kupunguza kero kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Godwin Gondwe wakati akitoa tamko la jiji kwa waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wananchi kufuatia maandamano ya hapo jana ya wanachi wa Mtaa ya Miuji walioandamana katika ofisi za jiji la Dodoma wakishinikiza wasikilizwe kero zao juu ya masuala ya ardhi ikiwemo swala la kubomelewa nyumba zao.

Sauti ya Mh. Gondwe.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Godwin Gondwe ambae ni mkuu wa wilaya ya Bahi akuzungumza na waandishi wa habari. Picha na Fred Cheti.

Akizungumzia Mgogoro huo unaodaiwa kudumu kwa miaka 10 Mhe. Gondwe amesema kuwa itaundwa timu ya wataalamu wa ardhi wa jiji la Dodoma kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi hao ambayo itakaa ndani ya siku 7 na kupitia maeneo mbalimbali ya mgogoro huo ili kujua mahali pa kuanzia kwa ajili ya utatuzi wake.

Sauti ya Mh. Gondwe.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mtaa wa Miuji Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Amani Simba amewasihi wananchi wake kuwa watulivu kwani wapo sehemu sahihi na salama kwa ajili ya kusikilizwa kero zao.

Sauti ya mwenyekiti wa Miuji.