Dodoma FM

Bahi: Nollo kupeleka umeme, maji shule mpya ya Nagulo

6 July 2023, 4:50 pm

Mheshimiwa Nollo akizungumza na viongozi wa chama na serikali kijiji cha Nagulo. Picha na Bernad Magawa.

Nollo amesema kufanya hivyo kutaongeza thamani katika mradi huo ulioletwa na serikali kwa lengo la kuwasaidia wananchi.

Na Bernad Magawa

Mbunge wa jimbo la Bahi Mheshimiwa Kenneth Nollo ameahidi kupeleka huduma ya maji umeme pamoja na kuchonga barabara kuingia shuleni hapo ili kuwaondolea adha watumishi watakaofanya kazi shuleni hapo pamoja na wananchi wa kijiji hicho ambao wanakabiliwa na adha ya kukosa maji safi kwa matumizi ya nyumbani.

Mheshimiwa Nollo ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na viongozi wa kijiji cha Nagulo wilayani Bahi alipotembelea shule mpya  ya  Nagulo kwa ajili ya kuangalia upatikanaji wa huduma muhimu katika shule hiyo ili kuongeza thamani ya uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na serikali.

Sauti ya Mh Nollo.
Mheshimiwa Nollo akiwa na wananchi wa kijiji cha Nagulo Bahi alipotembelea majengo ya shule mpya ya Nagulo. Picha na Bernad Magawa.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Nagulo Asheri Ujuku  akaeleza namna wananchi wa kijiji hicho wanavyopata adha kubwa ya kukosekana kwa maji kijijini hapo  huku wananchi wakiomba kuanza kutolewa huduma za afya katika jengo jipya la zahanati lililojengwa kijijini hapo.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji, na wananchi.

Awali mwalimu mkuu wa Shule ya Nagulo Bahi Richard Chuma alipata fursa ya kueleza changamoto zinazoikabili shule hiyo na kufikisha ombi kwa Mbunge ili kupatiwa ufumbuzi.

Sauti ya Mwalimu mkuu wa Shule ya Nagulo Bahi.