Dodoma FM

Senyamule akabidhiwa miradi ya BOOST wilayani Bahi

5 July 2023, 3:31 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule akiwa ameambatana na viongozi wengine kukagua miradi hiyo.Picha na Bernad Magawa.

Senyamule amepongeza uongozi wa wilaya ya Bahi kwa mshikamano ambao umewafanya kuwa wa kwanza kukamilisha miradi hiyo.

Na Bernad Magawa

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule amekabidhiwa jumla ya madarasa 51, vyoo 63, majengo 2 ya utawala  pamoja na nyumba ya mwalimu moja yenye uwezo wa kukaa familia mbili  wilayani Bahi vyote vikiwa na gharama ya  shilini Billion 1.5 fedha kutoka serikali kuu (BOOST) baada ya miradi hiyo kukamilika.

Akizunungumza wakati  wa kuweka jiwe la msingi shule mpya ya msingi Bahi Misheni ikiwakilisha miradi yote ya BOOST wilayani humo  Senyamule amepongeza uongozi wa wilaya ya Bahi kwa mshikamano ambao umewafanya kuwa wa kwanza kukamilisha miradi hiyo  kwenye Mkoa wa Dodoma huku katibu tawala wa mkoa wa Dodoma Ally Gugu naye akitoa pongezi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule akiweka jiwe la msingi katika miradi hiyo. Picha na Bernad Magawa.

Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gongwe akimkaribisha Mheshimiwa Senyamule katika mradi huo ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan huku Mbunge wa jimbo la Bahi Kenneth Nollo na Mwenyekiti wa  halmashauri ya wilaya hiyo Donald Mejitii (MNEC) na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stuwart Masima  nao wakaeleza mambo mbalimbali.

Sauti ya Viongozi wa wilaya.

Awali Afisa elimu ya awali na msingi wilaya ya Bahi Boniface Wilson alieleza namna madarasa hayo yatakavyo punguza msongamano wa wanafunzi madarasani huku Diwani wa kata ya Bahi Agostino Ndonuu pamoja na mwenyekiti wa kijiji cha Bahi sokoni Sifaeli Mbeti wakizungumza kwa niaba ya wananchi.

Sauti za Afisa elimu, diwani , mwenyekiti wa kijiji.