Dodoma FM

Nollo atatua changamoto ya huduma za afya Mapinduzi Kigwe

4 July 2023, 3:49 pm

Wananchi pamoja na mbunge wa jimbo la Bahi wakishiriki katika ujenzi wa zahanati ya Mapinduzi. Picha na Bernad Magawa.

Uwepo wa huduma za afya kwenye kila kijiji wilayani Bahi mkoani Dodoma kutawahakikishia wananchi wa wilaya  hiyo usalama wa afya zao  pindi watakapopatwa na maradhi mbalimbali.

Na Bernad Magawa.

Mbunge wa jimbo la Bahi Mhe.  Kenneth Nollo ametoa zaidi ya shilling million 16  katika ujenzi wa zahanati ya  Mapinduzi kata ya Kigwe ili kuwaondolea changamoto wananchi wa kijiji hicho kufuata huduma za afya umbali mrefu.

Akizungumza wakakati wa  kikao kwenye kata ya Kigwe Mheshimiwa Nollo amesema pamoja na mfuko wa jimbo halmashauri ya wilaya ya Bahi pia imepanga kupeleka fedha  kwa mwaka huu wa fedha kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika ili kuanza kutoa huduma.

Sauti ya Mheshimiwa Kenneth Nollo.
Wananchi pamoja na mbunge wa jimbo la Bahi wakishiriki katika ujenzi wa Zahanati hiyo ya Mapinduzi. Picha na Bernad Magawa.

Nollo amesema kwa muda wa miaka miwili ambao yeye amekuwa madarakani kama Mbunge wa  Jimbo la Bahi, amebakisha vijiji viwili tu kati ya 16 ambavyo havikuwa na huduma za afya wakati anaingia madarakani huku akiahidi kukamilisha vjijiji vyote kabla ya 2025.

Sauti ya Mheshimiwa Kenneth Nollo.