Dodoma FM

Makatibu tawala watakiwa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia utawala bora

4 July 2023, 6:11 pm

Makatibu Tawala wa Wilaya wakiwa katika semina elekezi iliyoanza leo julai 4 hadi julai 6 katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma. Picha na Mindi Joseph.

Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Ungozi yamehusisha Makatibu Tawala wa Wilaya 135 za Tanzania Bara.

Na Mindi Joseph.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Makatibu Tawala wa Wilaya zote Tanzania Bara watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia utawala bora, miiko na maadili ya viongozi wa umma.

Ametoa maagizo hayo leo Jumanne, Julai 04, 2023 wakati akifungua semina elekezi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma.

Sauti ya Waziri mkuu.
Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akuzungumza wakati akifua semina elekezi kwa makatibu tawala hao wa wilaya.Picha na Mindi Joseph.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema lengo ya mafunzo hayo ni kuongezea weledi kwa viongozi hao ili kuimarisha utawala bora.

Sauti ya waziri Simbachawene.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angela Kairuki amewataka viongozi hao watimize majukumu yao ipasavyo na wahakikishe wanasimamia utekelezaji wa maagizo ya viongozi katika maeneo yao ya kazi.

Sauti ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.