Dodoma FM

Wizara ya Ardhi yajadili namna ya kumaliza migogoro ya ardhi Dodoma

30 June 2023, 4:34 pm

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao hicho .Picha na Mindi Joseph.

Juni 30 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula atakutana na wananchi jijini Dodoma Kusikiliza changamoto za upatikanaji wa hatimiliki ya ardhi.

Na Mindi Joseph.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekutana na watendaji wa wizara yake kuweka mikakati na kuangalia namna ya kumaliza Migogoro ya ardhi katika jiji la Dodoma.

Waziri Mabula ameyasema hayo jijini Dodoma ambapo ameainisha kuwa hadi sasa vijiji vingi vimepimwa ila changamoto iliyopo ni mpango wa matumizi ya ardhi haujavifikia.

Sauti ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi .
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo . Picha na Mindi Joseph.

June 28 wakati waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitaka malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kwenye maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya jiji  la Dodoma yalipwe fidia kwa wakati ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza siku za usoni.

Sauti ya waziri Mkuu Kassim Majaliwa.