Dodoma FM

Dodoma: Wafanyabiashara waomba kuboreshewa mazingira

30 June 2023, 5:02 pm

Wafanyabiashara hao wanalalamika uwepo wa chemba ya maji taka katika eneo hilo ambayo inavujisha maji yanayo zagaa katika eneo hilo.

Katika eneo hilo zipo daladala zinazoelekea maeneo mbalimbali nje ya jiji ikiwemo Mpunguzi ambapo pia wapo baadhi ya akina mama na wafanyabiashara wadogo wanaojishughulisha na biashara katika eneo hili ingawa hali ya upatikanaji wa wateja sio ya kuridhisha.

Na Thadei Tesha.

Wafanyabiashara pamoja na madereva wa Daladala katika kituo kilichopo nyuma ya machinga complex jijini Dodoma wameiomba serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kituo hicho ili kuvutia wafanyabiashara pamoja na wasafiri kufika katika eneo hilo.

Dodoma Tv imefanya mahojino na baadhi ya wafanyabiashara pamoja na madereva wa daladala katika eneo hilo kutaka kufahamu mwenendo wa hali ya biashara ilivyo kwa sasa katika kituo hicho ambapo wamesema kuwa ni vyema serikali ikaweka miundombinu rafiki itakayosaidia wao kuzidi kupata wateja kama wanavyoeleza.

Sauti za wafanyabiashara .