Dodoma FM

Milioni 560 kutatua kero ya maji Bahi

28 June 2023, 5:41 pm

Wakazi wa Kijiji cha Nagulo Bahi wakiwa katika Mkutano . Picha na Mindi Joseph.

Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama umeendelea kuwa changamoto katika baadhi ya vijiji mkoani Dodoma.

Na Mindi Joseph.

Milioni 560 zinatarajiwa kutumika katika kuchimba kisima cha maji ndani ya kijiji cha Uhelela wilayani Bahi mkoani Dodoma ambacho kitahudumia wakazi wa Nagulo wanaokabiliwa na changamoto ya maji.

Akizungumza na Taswira ya Habari, diwani wa kata ya Bahi Augostino Ndonu amesema kijiji cha Nagulo Bahi  kinakabiliwa na ukosefu wa kisima cha maji safi na salama ya kunywa.

Ameongeza kuwa uchimbaji wa kisima hicho cha maji utasaidia kuleta ahueni kwa wakazi hao.

Sauti ya Diwani wa kata ya Bahi.
Diwani wa kata ya Bahi Mh. Agostino Ndunu akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Nagulo Bahi katika Mkutano huo. Picha na Mindi Joseph.

Mbunge wa jimbo la Bahi Dodoma Mhe. Kenneth Nollo anasema lengo la uchimbaji wa visima ni kuendelea kutatua changamoto ya maji kwa wananchi huku wananchi wa Asanje pia wakitarajia kuchimbiwa kisima cha maji.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Bahi.