Dodoma FM

Jamii inaamini nini kuhusu waraibu wa dawa za kulevya?

28 June 2023, 2:30 pm

Mkazi wa jiji la Dodoma akizungumza na Dodoma Tv kuhusu waraibu wa dawa za kulevya. Picha na Respishas Lopa.

Maadhimisho ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya yalifanyika kitaifa mkoani Arusha Juni 25 mwaka huu.

Na Respishas Lopa.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wameonesha utayari wao wa kuwapokea waraibu wa dawa za kulevya na kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za maendeleo iwapo watabadilika na kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Wamesema hayo wakati wakizungumza na Dodoma Tv juu ya mchango wao katika kushirikiana na waraibu wa dawa za kulevya walioamua kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Wananchi hao wamesema jamii haina budi kuwapokea na kuwapa ushirikiano kwani ni njia mojawapo ya kuwasaidia kutoshawishika kurejea katika matumizi ya dawa za kulevya.

Sauti za wananchi.
Mkazi wa jiji la Dodoma akizungumza na Dodoma Tv kuhusu waraibu wa dawa za kulevya. Picha na Respishas Lopa.

Mmoja wa waraibu wa dawa za kulevya kutoka Jijini Dodoma amesema kitendo cha wao kutengwa na jamii kina sababisha kujiona wapweke licha ya kuwa na dhamira ya dhati kuachana na mdawa hzo.

Sauti ya mmoja wa waraibu.

Juni 25 mwaka huu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akihutubia katika kilele cha siku ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya mkoani Arusha alitoa wito kwa vikundi vya sanaa kuwekeza nguvu katika kuelimisha jamii juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya.

Sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.