Dodoma FM

Serikali yaondoa tozo miamala ya kutuma fedha kwa njia ya simu

27 June 2023, 6:28 pm

Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule katika uzinduzi wa ofisi mpya za Vodacom Jijini Dodoma. Picha na Mindi Joseph.

Mkoa wa Dodoma umebahatika kupata minara 36 huku 6 ikijengwa na Vodacom.

Na Mindi Joseph.

Serikali imeondoa tozo kwenye miamala ya kutuma fedha katika mitandao mbalimbali ya simu ili kuondoa adha kwa watazania.

Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye katika uzinduzi wa ofisi mpya za Vodacom jijini Dodoma amesema Rais Samia ameridhia kuondoa tozo za kutuma miamala kwa njia ya simu hadi  asilimia 0.

Sauti ya mh.Nape Nnauye .

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso amesema sekta ya mawasiliano inatengeneza uchumi wa nchi.

Sauti ya Mh. Selemani Kakoso.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo . Picha na Mindi Joseph.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amebainisha kuwa mkoa wa Dodoma umebahatika kupata minara 36 huku 6 ikijengwa na Vodacom

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema Vodacom wamepeleka minara  hadi vijijini ili kurahisi mawasiliano kwa wananchi na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.