Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuwajali watoto wenye ulemavu

26 June 2023, 12:17 pm

Wakazi wa kijiji cha Nagulo Bahi wakiwa katika mkutano kwa ajili ya kupata elimu ya lishe. Picha na Mariam Kasawa.

Wazazi wanakumbushwa kuendelea kuwajali watoto wenye ulemavu kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao muhimu ili waweze kutimiza ndoto zao.

Na Mariam Kasawa.

Wazazi wametakiwa kuwajali na kuwathamini watoto wenye ulemavu kwa kuwapatia elimu ili waweze kutimiza ndoto zao .

Ni katika maadhimisho ya wiki ya lishe yaliyowakutanisha wahudumu wa afya, viongozi wa kata ya Bahi na wakazi wa Nagulo Bahi ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa makundi matano ya chakula.

Akizungumza na wakazi wa Nagulo Bahi, diwani wa kata ya Bahi Agostino Ndunu amewataka wakazi hao kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu na endapo wanafahamu uwepo wa mtoto yeyote mwenye ulemavu aliyefichwa watoe taarifa kwa uongozi.

Sauti ya Diwani wa kata ya Bahi.
Diwani wa kata ya Bahi Agostino Ndunu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nagulo Bahi. Picha na Mariam Kasawa.

Bi. Jane Mdigane ni mratibu wa mradi wa elimu jumuishi kutoka kanisa la FPCT yeye amewataka wazazi kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao pamoja na kuwapatia haki ya elimu watoto wenye ulemavu.

Sauti ya Mratibu wa Mradi wa Elimu jumuishi kutoka kanisa la FPCT.

Baadhi ya wazazi wenye watoto wenye ulemavu wamesema wazazi wanatakiwa kuwajali watoto wenye ulemavu kwani watoto hao ni tunu kutoka kwa Mungu hivyo wanatakiwa kuwajali na kuwathamini.

Sauti ya mzazi .