Dodoma FM

NEMC, TBS zakutana kujadili katazo vifungashio vya plastiki

26 June 2023, 1:37 pm

Kikao kazi baina ya NEMC na TBS walivyokutana kujadili kuhusu utekelezaji wa katazo matumizi ya vifungashio visivyokidhi ubora. Picha na Fred Cheti.

Vifungashio visivyo kidhi ubora vinatajwa kuleta athari katika mazingira.

Na Fred Cheti.

Baraza la uhifadhi na usimamizi wa  mazingira (NEMC) limekutana na shirika la viwango nchini (TBS) na kufanya kikao kazi kwa lengo la utekelezaji wa katazo la matumizi ya vifungashio visivyokidhi ubora.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria za mazingira kutoka katika baraza hilo Bi. Redempta Samuel ameelezea lengo  la kuwa na kikao hicho.

Sauti ya mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria za mazingira .
Afisa viwango kutoka katika shirika hilo la viwango nchini (TBS) Bwana Henry Msuya akizungumza kuhusu kikao kazi hicho. Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake afisa viwango kutoka katika shirika hilo la viwango nchini (TBS) Bwana Henry Msuya anaelezea jinsi ambavyo wamepanga kushirikiana na (NEMC) katika kupunguza matumizi ya vifungashio ambavyo vinatajwa kuwa na athari katika mazingira.

Sauti ya Afisa viwango kutoka TBS.