Dodoma FM

Wakulima wa alizeti Bahi walalamika kuporomoka kwa bei

21 June 2023, 3:47 pm

Kupungua kwa ubora wa zao la alizeti kwa msimu huu kumesababisha bei yake kuwa chini kuliko msimu uliopita. Picha na Blog.

Wakulima hao wanasema wanalazimika kuuza alizeti kwa bei ndogo ili waweze kupata fedha za kujikimu .

Na Bernad Magawa.

Wakulima wa zao la alizeti wilayani Bahi wamelalamikia kuporomoka kwa bei ya zao hilo ambalo limejipatia umaarufu hivi karibuni na kuwa miongoni mwa mazao ya kibiashara mkoani Dodoma .

Wakizungumza na kituo hiki wakulima hao wamesema hakuna soko maalum la kuuzia zao hilo hali inayowalazimu  kuuza kwa bei ndogo ili  waweze kupata fedha za kujikimu ambapo hulazimika kuuza kwa bei ya shilingi 600 kwa kilo moja hali inayomdidimiza mkulima .

Sauti za wakulima.

Kwa upande wao baadhi ya wanunuzi wa zao hilo wilayani Bahi wamesema kupungua kwa ubora wa zao la alizeti kwa msimu huu umesababisha bei yake kuwa chini kuliko msimu uliopita kwani alizeti ni nyepesi sana kiasi cha kushindwa kukidhi ubora unaotakiwa.

Sauti za wanunuzi wa Alizeti.

Abisa Lungwe ni Afisa ugani wa kata ya Lamaiti wilayani Bahi  anatoa ushauri kwa wakulima wa alizeti katika kukabiliana na tatizo la bei ndogo ya zao hilo huku akieleza kitaalam sababu zilizosababisha zao hilo kukosa ubora wa kutosha katika msimu huu.

Sauti ya Afisa Ugani.