Dodoma FM

Uboreshaji miundombinu Bahi wawakomboa mama lishe

16 June 2023, 2:53 pm

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mh. Godwin Gondwe akiongea na mama lishe. Picha na Bernad Magawa.

Uwepo wa miradi mingi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya wilayani Bahi  umeongeza fursa ya vijana na akina mama ambao baadhi yao wameshiriki moja kwa moja katika kazi za ujenzi, na  wengine kuuza vifaa vya ujenzi katika miradi hiyo kama vile  matofali, mchanga pamoja na madirisha.

Na Bernad  Magawa.

Baadhi ya mama lishe wilayani Bahi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka miradi ya ujenzi wilayani Bahi kwani imewawezesha kujipatia kipato.

Mama lishe hao wamesema pamoja na lengo la serikali kuboresha miundombinu ya elimu, pia wao wamenufaika kupitia kuuza chakula kwa mafundi wanaojenga miradi hiyo.

Sauti ya Sauti ya Mama lishe.

Akizungumza na wajasiriamali hao, mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe amewaasa akina mama hao kuitumia fursa hiyo vizuri ili waweze kutimiza malengo yao.

Sauti Godwin Gondwe  Mkuu wa wilaya ya Bahi.