Dodoma FM

Dodoma: Wafanyabiashara watakiwa kujiunga UBIMIDO

14 June 2023, 4:53 pm

Baadhi ya akina mama katika biashara ya mzao. Picha na Thadei Tesha.

Umoja wa wafanyabiashara waendao mnadani umekuwa na umuhimu mkubwa hususani katika suala la kuwasaidia wafanyabiashara katika kusaidiana kwenye masuala mbalimbali.

Na Thadei Tesha

Wafanyabiashara jijini Dodoma wametakiwa kujiunga katika umoja wa wafanyabiashara UBIMIDO ili waweze kupata fursa za kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika mambo mbalimbali.

Hayo yamesemwa na katibu wa umoja wa wafanyabiashara waendao minadani jijini hapa Bw. Julias Petro katika mahojinao maalum na Dodoma Tv ambapo kwanza anaanza kwa kuelezea juu ya fursa zilizopo kwa wafanyabiashara waliojiunga katika umoja huo.

Sauti ya katibu wa umoja wa wafanyabiashara waendao minadani
katibu wa umoja wa wafanyabiashara waendao minadani jijini Dodoma Bw. Julias Petro .Picha na Thadei Tesha.

Pamoja na umuhimu huo zipo baadhi ya changamoto zinazowakabili katika umoja huo hapa mwenyekiti wa umoja huo Bw. Faustine Fransis anaelezea baadhi ya changamoto hizo.

Sauti ya katibu wa umoja wa wafanyabiashara waendao minadani

Kwa upande wao baaadhi ya wananchi waliojiunga na umoja huo wanaelezea walivyonufaika na umoja wa wafanyabiashara huku wakitoa ushauri juu ya watu kujiunga na umoja huo.

Sauti za wafanyabiashara.