Dodoma FM

Vituo vya afya vyatakiwa kununua majokofu ya kuhifadhia mazao ya damu

14 June 2023, 6:00 pm

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu akizungumza leo katika uzinduzi wa kituo cha damu salama. Picha na Mindi Joseph.

Tanzania leo imeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya Wachangia Damu Duniani ambayo inalenga kuongeza ufahamu na kuwashukuru wafadhili wa damu wa hiari, wasiolipwa kwa zawadi zao za kuokoa maisha.

Na Mindi Joseph.

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu ametaka vituo vyote vya afya vya serikali  nchini kununua majokofu ya kuhifadhia mazao ya damu.

Waziri Ummy ameyasema hayo katika uzinduzi wa huduma za damu salama kituo cha Kanda ya Kati Dodoma siku ya wachangia Damu Duniani.

Sauti ya Waziri wa Afya.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amesema uchache wa vituo umechangia kutotengeneza mazao ya damu.

Sauti ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Dk. Neema Kileo anaainisha kuwa utafiti unaonesha kuwa vifo 43 kati ya 100 vinasababishwa na wanawake kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua.

Sauti ya Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini .