Dodoma FM

Wananchi Mpwayungu waishukuru serikali kwa kuboresha barabara

7 June 2023, 6:53 pm

Ukarabati wa barabara ukifanyika. Picha na Victor Chigwada.

Katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa dodoma ukarabati wa miundombinu mbalimbali umekuwa ukifanywa ambapo imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza changamoto ya usafiri .

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa kata ya Mpwayungu iliyopo katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wameishukuru serikali kwa juhudi za kuboresha miundombinu ya barabara inayounganisha vijiji  na miji hapa nchini.

Pongezi hizo wamezitoa wakati wakizungumza na Taswira ya Habari ambapo baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa  barabara nyingi ndani ya kata hiyo zimefanyiwa maboresho na zingine mpya kufunguliwa.

Sauti za wananchi.

Aidha wameiomba serikali kupitia wakandarasi wa miundombinu hiyo kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika ili kuleta tija katika ujenzi wa barabara hizo.

Naye diwani wa kata ya Mpywayungu Bw. Antony Sakalani amekiri serikali kuendelea kutoa fedha za miundombinu licha ya baadhi ya maeneo kuendelea kuwa changamoto.

Sauti ya Diwani.

Sakalani ameongeza kuwa ni vyema serikali kutenga bajeti ya fedha kwa ajili ya ukarabati wa maeneo korofi.

Sauti ya Diwani.